Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari ya kujiuguza ya Rama Akudo

48159 Pic+akudo

Sat, 23 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Leo mzima lakini kesho unaweza kuwa kitandani ukipigania uhai wako. Ndivyo anavyoanza kueleza Meneja wa bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’, Ramadhani Pesambili ‘Rama Akudo’, ambaye kwa sasa yuko kitandani akiugua.

Akiwa nyumbani kwake Mwananyamala A jijini Dar es Salaam, anasema alianza kuumwa akiwa Dodoma kwenye shoo ya Akudo Impact Februari mwaka jana, ambako alihisi mguu kama umestuka.

“Kwa kweli sijajua uhai wangu utakuwaje hapo baadaye, maana hata ninachoumwa sijajua hadi sasa. Nilianza kama masihara tu mwaka jana nilipokuwa Dodoma kwenye shoo ya Akudo, mguu wangu wa kulia ulistuka nikapata maumivu makali. Baada ya muda maumivu yalipungua na kuendelea na shughuli nyingine, nikarudi nyumbani Dar es Salaam nikiwa salama kabisa.

Anasema baada ya kupata matibabu ya wali ilikugundulika kuwa ana usaha kwenye nyonga na kulazimisha kufanyiwa upasuaji wa kuutoa. Rama ambaye alianza kuisimamia bendi ya Akudo mwaka 2012, aliongeza; “Baada ya upasuaji huo wa kwanza, nilipata nafuu kidogo tofauti na yale maumivu ya mwanzo niliyokuwa nayasikia. Lakini kadri siku zilivyozidi kwenda hali ilibadilika tena ikabidi nipelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Tawi la Mloganzila.

Pale nilianza kuchukuliwa vipimo upya. Wakachukua kinyama sehemu ya nyonga na kuambiwa nisubiri majibu baada ya wiki moja. Hata hiyo, hakufanikiwa na kulazimika kuhamia katika hospitali nyingine.

Amekuwa akihangaika na matibabu ambayo yanamgharimu fedha nyingi hasa ukizingatia kuwa hana namna nyingine ya kuingiza pesa.

Anasema watakaoguswa na hali ngumu anayopitia hivi sasa watamfariji sana kama wakimchangia ili aweze kuendelea kupambana kujaribu kuokoa maisha yake.

“Kwa watakaoguswa na kutaka kunipatia msaada basi watume tu kwenye namba hizi 0715-862051 hii ni Tigo na Voda ni 0764888840 jina ni Rama Pesambili, Mungu aendelee kuwabariki sana na naomba maombi yenu,” anasema Rama Akudo.



Chanzo: mwananchi.co.tz