Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sadaka zaibiwa Kanisa Katoliki, Padre atoa kauli nzito

Sadaka Church E.jpeg Sadaka zaibiwa Kanisa Katoliki, Padre atoa kauli nzito

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paroko wa Parokia ya Narumu, Kata ya Machame Mashariki, Padri Thomas Chuwa amelaani vikali katika ibada ya Misa Takatifu kitendo kilichofanyika katika Ibada ya Jumapili iliyopita ambapo watu / mtu wasiojulikana wameiba kapu la sadaka kanisani.

Sadaka hizo zilikuwa ni majitoleo ya shukrani, vipaji pamoja na sadaka ya Misa Takatifu katika Ibada ya Misa ya kwanza ya Jumapili iliyopita.

Padri Chuwa amewaasa waamuni wa kanisa hilo kusali Sala Maalum kwa muda wa siku tatu kwa ajili ya watu/mtu huyo aliyeiba sadaka hizo na kuwa kitendo hicho kilichofanyika kanisani hapo ni kibaya sana na anamkabidhi Mungu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live