Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za kupungua uhalifu Arusha zatajwa

30393 UHALIFU+PIC Kamanda wa polisi mkoani hapa, Ramadhani Ng’anzi

Thu, 6 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Kamanda wa polisi mkoani hapa, Ramadhani Ng’anzi amesema kuwa, Mkoa wa Arusha kwa sasa hivi matukio mbalimbali ya uhalifu yakiwemo ya ujambazi yamepungua kutokana na kuimarishwa Kwa ulinzi na usalama Kwa kiwango cha juu.

Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na mwananchi ofisini kwake kuhusiana na kupungua kwa matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyokuwa yakitikisa jiji la Arusha.

Kamanda Ng’anzi alisema kuwa, kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu januari mwaka huu hadi desemba matukio ya uhalifu yamepungua kutokana na ulinzi wa hali ya juu ulioimarishwa kutoka kwa polisi wenyewe kwa kushirikiana na wananchi kwa ujumla.

Alisema kuwa, swala la ulinzi kuimarishwa mkoani hapa ni la lazima kutokana na kuwa Arusha ni alama ya utalii , kutokana na kuwepo Kwa wageni wengi wa mataifa wanaofanya kazi maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Aliongeza kuwa, Mkoa wa Arusha umekuwa ukisifika kiuchumi kutokana na kuwepo Kwa viwanja mbalimbali vya ndege ambavyo vinatumika na wageni wa kimataifa hali inayopelekea ulinzi kuimarishwa Kwa kiwango cha juu.

Alisema kuwa, jeshi hilo limejiwekea mikakati katika kufanya doria mbalimbali Kwa kutoa ulinzi Kwa wageni na watalii ikiwemo doria za miguu, magari na mbwa katika maeneo mbalimbali ambayo imesaidia kuimarisha ulinzi Kwa kiwango kikubwa Sana.

“sasa hivi polisi wetu wametoka kambini na kwenda mtaani Kwa wananchi kusikiliza matatizo yao ya kiusalama hivyo tumekuwa tukiwafuata wananchi hukohuko walipo badala ya kukaa kambini kila wakati huku tukitumia ulinzi shirikishi katika mitaa mbalimbali iliyokuwa umeshindikana na kupewa majina ya mtaa wa” jambazi” ambapo sasa Hivi yanaitwa mtaa wa “amani”. “alisema Kamanda.

Aidha aliongeza kuwa, jeshi hilo limekuwa mstari wa mbele kufika eneo la tukio pindi uhalifu unapotokea ambapo ndani ya dakika 30 polisi wanakuwa wameshafika eneo la tukio na kusimamia kikamilifu tukio hilo kuanzia mwanzo hadi Mwisho.

Kamanda alisema kuwa, wamejiwekea mkakati wa kuhakikisha kuwa, kila alipo mwananchi na polisi wapo sambamba na kumjali mteja katika kuhakikisha anapata huduma iliyo bora na ya kuridhisha pia.

Aidha alitoa wito kwa wananchi pamoja na wadau mbalimbali kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi hilo katika kufichua wahalifu mbalimbali ili jiji la Arusha liendelee kubaki salama Kwa manufaa ya wananchi wetu pamoja na wageni Kwa ujumla.



Chanzo: mwananchi.co.tz