Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za kufanya kazi mazingira hatarishi zatajwa

40011 Pic+afya Sababu za kufanya kazi mazingira hatarishi zatajwa

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ukosefu wa kozi maalumu ya usalama na afya katika sehemu za kazi katika vyuo vikuu hapa nchini imeelezwa kuchangia waajiriwa kufanya kazi katika mazingira hatarishi.

Hii ni kutokana na ukosefu wa vifaa vya kujikinga hivyo kupelekea kuhatarisha afya zao. 

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Februari 4, 2019 na mtendaji mkuu wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (Osha), Khadija Mwenda, wakati akifungua mafunzo kuhusu usalama na afya mahali pa kazi.

Mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa juu ya usalama na afya sehemu ya kazi kwa wafanyakazi walioajiriwa katika taasisi, mashirika ya umma na sekta binafsi.

Mwenda amesema usalama mahala pa kazi katika vyuo vikuu inafundishwa kama somo lakini haimuwezeshi mhitimu kupata cheti maalumu.

"Ifahamike kuwa huu ni mtaala kama ilivyo mitaala mingine hivyo sioni sababu kwa nini kusiwe na kozi hii maalimu ambayo mwanafunzi atasoma na akapata cheti chake maalumu," amesema.

Akizungumizia usalama na afya mahala pa kazi amesema  ukizingatiwa ipaswavyo unaongeza tija kwa mwajiri na waajiriwa na hivyo kuongeza uzalishaji.

"Hata hivyo mikakati yetu ni kutengeneza programu ya pamoja katika vyuo mbalimbali nchini ili kuona namna gani somo hili linakuwa kozi maalumu," amesema.

Mfanyakazi kutoka mgodi wa madini mkoani, Geita Zaituni Dodo anayepata mafunzo hayo amesema baada ya mafunzo hayo atakwenda kuelimisha wafanyakazi wenzake jinsi ya kujikinga na madhara yatokanayo na ukosefu wa usalama kazini.

Mafunzo hayo yanahusisha wataalamu mbalimbali na wahitimu wa elimu ya juu wanaotarajia kuanza kazi katika taasisi mbalimbali.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz