Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu uhaba wa maji zawekwa wazi

MAJII Sababu uhaba wa maji zawekwa wazi

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya imesema ongezeko la watu na wawekezaji wa viwanda kumechangia uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo huku mahitaji yakiwa lita milioni 90 lakini uzalishaji ni lita milioni 65 kwa siku.

Mwenyekiti wa bodi ya maji, Edna Mwaigomole amesema hayo leo Jumatatu Oktoba 10,2022 wakati akizungumza na wenyeviti na watendaji katika kata 36 za Jiji la Mbeya sambamba na kutembelea chanzo cha maji Nzovwe na mabwawa ya uchakataji wa mifumo ya maji taka katika eneo la Itende jijini hapa ''Kumeka na adha ya maji katika baadhi ya maeneo tatizo kubwa ni ongezeko la watu, “ amesema

Amesema kutokana na hadha wanaendelea kuboresha vyanzo vya maji sambamba utekelezaji wa mradi wa kimkakati kutoka mto Kiwira Wilaya ya Rungwe ambao utakuwa mwarobaini wa tatizo la maji Mwaigomole ametaja changamoto nyingine ni matumizi holela, wizi, shughuli za kijamii kwenye vyanzo vya maji ikiwepo na upotevu wa maji ambao jamii imekuwa ikishindwa kutoa taarifa katika mamlaka husika.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja , Neema Neema Mangwala amesema kuwa kuna uhaba wa maji kwa asilimia 62 huku mahitaji asilimia 100 na upungufu wa asilimia 38 sambamba na wananchi kushindwa kulipa ankara za maji kwa wakati ambapo zaidi ya Sh 3.2 ni malimbikizo ya madeni.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Saimon Bukuku amesema ili kufikia malengo ni wakati sasa watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kuhamasisha jamii kujua umuhimu wa kutunza rasilimali ya maji na kulipa ankara kwa wakati.

Mwenyekiti wa Mtaa wa bombs mbili Kata ya Mwakibete, Rodrick Mwang'onda amesema kuwa watakuwa mabalozi wa kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa ili kuondoka na hadha ya maji katika Mitaa jijini hapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live