Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saba wafariki ajali ya basi Lindi

Saibaba Ajali Lindi (600 X 321) Saba wafariki ajali ya basi Lindi

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu saba wamefariki dunia na wengine 22 kujeruhiwa katika ajali ya iliyohusisha mabasi mawili katika kijiji cha Kiwawa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

Akizungumza leo Ijumaa Oktoba 6, 2023, Kamanada wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Pili Mande amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana mnamo majira ya saa 8 mchana katika kijiji cha Kiwawa Wilaya ya Kilwa, ambapo lihusisha gari aina ya Scania mali ya kampuni ya Saibana linalofanya safari zake Nachingwea kwenda Dar es saaalam liligongana na gari la kampuni ya Baharia linalofanya safari zake Dar es salaam kwenda Tandahimba mkoani Mtwara.

Kamanda huyo amesema kuwa kwenye ajali hiyo dereva wa basi la Saibaba alietambuliwa kwa jina la Lucas John (59) mkazi wa Arusha amefariki hapo hapo pamoja na dereva wa basi la kampuni ya Baharia alietambuliwa kwa jina la Omary Abdalla (47) mkazi wa jijini Dar es Salaam.

"Waliofariki hapo hapo madereva wawili pamoja na abiria watano ambao miili yao bado haijatambuliwa hadi sasa, miili imehifadhiwa katika hosptali ya Kinyonga iliyopo Wilayani Kilwa Mkoani lindi," amesema Kamanda Mande.

Majeruhi 22 kati ya hao watatu hali zao ni mbaya na majina yao hayajafahamika, ambao ni wanawake wawili na mtoto mmoja wa kiume wote wamelazwa katika hosptali ya Kinyonga iliyopo Wilayani Kilwa.

Amesema majeruhi wengine 19 wanaendelea kutibiwa na kuangaliwa afya zao kama wataendelea vuzuri wataruhusiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live