Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saba wadakwa wakidaiwa kujifanya maofisa usalama Tanzania

91078 Pic+usalama+feki Saba wadakwa wakidaiwa kujifanya maofisa usalama Tanzania

Wed, 8 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza nchini Tanzania kwa kushirikiana na vyombo vingine vya kiusalama limewakamata watu saba waliojifanya ni maofisa wa usalama wa Taifa kutoka Ikulu ya nchini hiyo.

Watu hao wanatuhumiwa kuwatapeli wananchi na watumishi wa Serikali huku wakiwajengea hofu ili kutengeneza mazingira ya kupewa rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Januari 7, 2020, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Murilo amesema matukio hayo yametokea kati ya Desemba 27, 2019 na Januari 2, 2020 maeneo ya Nyakato wilayani Nyamagana Mkoani hapa.

Murilo amesema watuhumiwa hao walikuwa wakitumia Gari aina ya Toyota la kubeba wagonjwa yenye usajili wa namba T.751 BNL ambalo walisema ni sehemu ya msafara wa viongozi wakuu.

"Walikamatwa na makachero na wakaendelea kujitambulisha kuwa wao ni maofisa usalama wa Taifa toka Ikulu lakini walipohojiwa kwa kina ilibainika ni matapeli" amesema Murilo.

Amewataja watuhumiwa hao saba kuwa ni; Chalanga Chalanga (45) mkazi wa Pansiansi Mwanza na Arusha, Hamis Mwalimu (25), Philipo Petro (35) mkazi wa Misungwi, Elia Gunda (30) mkazi wa Kisesa, Hassan Juma (29) mkazi wa Mkolani, Selemani Karanga (25) ambaye alijifanya mlinzi wa Chalanga Chalanga na Michael Mazigemkazi mkazi wa Morogoro.

>Murilo amesema watuhumiwa wamehojiwa, upelelezi ukikamilika watafikishwa Mahakamani.

Chanzo: mwananchi.co.tz