Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ST Francis wamtaja Mungu katika mafanikio yao

38307 Shulepic ST Francis wamtaja Mungu katika mafanikio yao

Fri, 25 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mungu, bidii, kujituma kwa walimu pamoja na wanafunzi zimetajwa kuwa sababu za ufaulu mzuri kwa wanafunzi wa shule ya sekondari St. Francis iliyopo mkoani Mbeya.

Shule hiyo ya wasichana imefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne iliyofanyika mwaka jana ikiwa na ufaulu wa daraja la kwanza kwa wanafunzi wote.

Akizungumza na MCL Digital leo kwa niaba ya mkuu wa shule hiyo mwalimu wa nidhamu, Neema Kimani amesema Mungu kuwa wa kwanza na kujituma kwa walimu na wanafunzi, imekuwa  chachu ya mafanikio hayo makubwa

"Tumekuwa tukimtanguliza Mungu kila wakati na kuwalea kama watoto hivyo wanakuwa huru kwetu na kueleza shida zao," amesema Neema.

Leonard Peter mmoja wa walimu katika shule hiyo amesema nafasi hiyo ni muhimu na ina maana kubwa kwani matokeo ya mwaka huu ni bora kuliko miaka ya nyuma.

Atia Mwasongwe, mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo, amesema matokeo hayo yanawapa nguvu na kuona hakuna kitu kinachoweza kuzuia wao pia kufanya vizuri.



Chanzo: mwananchi.co.tz