Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda inafunga mpaka na DR Congo juu ya Ebola

69409 Ebola+pic%255C

Fri, 2 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Rwanda imefunga mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wiki moja baada ya kutangaza kuwa haitafanya hivyo, kufuatia uthibitisho wa kesi ya tatu ya Ebola katika mji wa karibu wa Goma.

Afisa wa serikali aliliambia The East African kwamba Wizara ya Afya itatoa maelezo zaidi juu ya kufungwa kwa mpaka lakini ilithibitisha kwamba hatua hiyo ilitokana na hofu ya kuenea kwa virusi vya Ebola.

Rais wa Kongo katika hotuba yake ya Alhamisi alisema,” msimamo wa Rwanda ni uamuzi wa pamoja" ambao utaathiri raia kutoka nchi zote mbili ambao hulazimika kuvuka mpaka kama sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Goma ni mji wenye watu milioni mbili na kitovu kikubwa cha usafirishaji, mpakani na mji wa Rwanda  Gisenyi, ambao una idadi ya zaidi ya watu 85,000. Watu wengi wana kazi upande mwingine wa mpaka wakati wengine wana makazi au hupeleka watoto wao katika shule ya mji wa karibu.

"Kimsingi, uamuzi wa pamoja wa viongozi wa Rwanda, utapelekea raia wa Rwanda kutoweza kwenda Goma na Wakongo kutoweza kutoka Gisenyi lakini wanazuiliwa kurudi nyumbani," ilisema taarifa hiyo.

 

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz