Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruti mpya Kigamboni, wenye daladala waitwa

Daladala Nauli Kupanda Daladala

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibitu Usafiri Ardhini (LATRA) inawakaribisha wasafirishaji kuomba leseni kwenye njia mpya za daladala Dar es Salaam ili kufikisha huduma kwa wananchi.

Wito huo unahusu mabasi yanayojidhi vigezo na kwa gari mpya ambazo hazijawahi kusajiliwa katika mfumo wa utoaji leseni wa PRIMS dereva husika atapaswa kuthibitishwa LaTRA.

Miongoni mwa ruti hizo ni toka Kinyerezi kuenda Simu 2000 kupitia barabara Mandela, Kibada stendi kwenda Mbezi Luis kupitia barabara ya Mandela, Darajani na Morogoro

Ruti zingine ni toka Kibada Stendi kuenda Simu 2000, Temeke Mwisho, Tabata Segerea, Tegeta Nyuki, Kigogo Sokoni na Kawe.

Kwa ruti zote hizo ujazo wa abiria ni kuanzia 25, kwa ufafanuzi zaidi wa ruti hizo na barabara zinapopita tazama hapa chini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live