Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rushwa ndio sababu miradi mingi kutokamilika-DC Moyo

IMG 20221214 WA0052 Rushwa ndio sababu miradi mingi kutokamilika-DC Moyo

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imewataka wadau wa maendeleo pamoja na Taasisi mbalimbali kuupitia mkakati wa kitaifa dhidi ya Rushwa na kujitathimini ili kuona namna gani wanashirikiana na katika kutokomeza vitendo vya rushwa nchini.

Akizungumza katika kongamano la kukuza maadili, na vita dhidi ya Rushwa mkoani Iringa, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa hatua ya kujitathimini mara kwa mara itasaidia kukuza maadili katika taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukemea na kuchukua hatua atakayejihusisha na vitendo vya rushwa.

Kiongozi huyo wa Wilaya ya Iringa alisema kuwa kuwepo kwa vitendo vya Rushwa kunaifanya serikali kushindwa kutekeleza ipasavyo jukumu lake la kuwahudumia wananchi kikamilifu, kwa kuwa baadhi ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kutumika isivyo sahihi kutokana na rushwa.

Moyo alisema kuwa Rushwa ni chanzo cha miradi mingi ya maendeleo yenye manufaa kwa jamii kutokukamilika kwa wakati huku akitumia jukwaa hilo kuwakumbusha wadau kuupitia mkakati wa kitaifa dhidi ya rushwa.

Alisema kuwa maadhimisho hayo ya siku ya maadili na haki za binaadam ni fursa nzuri kwa kila mmoja kujitafakari namana gani amezingatia maadili katika shughuli anazofanya ikiwemo ushiriki wake katika kupinga vitendo vya rushwa kwani uchumi wa nchi umekuwa ukidumazwa na vitendo hivyo vya rushwa.

Awali Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupamabana na Rushwa mkoa wa Iringa Domina Mkama akimkaribisha mgeni wa heshima ameeleza lengo la kongamano hilo kuzisaidia taasisi na jamii kufanya kazi bila kutoa au kupokea rushwa.

Aidha Kiongozi huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa Amewahimiza washiriki wa kongamano hilo wakiwemo wawakilishi kutoka klabu za wapinga rushwa vyuoni kuwahakikisha wanakuwa mabalozi wazuri katika vita dhidi ya Rushwa kwa kuielimishja jamii kutambua athari za rushwa kwa maendeleo ya taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live