Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rungwe yapata msaada wa vitabu vya Sh1.1 bilioni

Rungwe Pic Data Rungwe yapata msaada wa vitabu vya Sh1.1 bilioni

Sun, 19 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imekabidhiwa msaada wa vitabu 35,000 vyenye thamani ya Sh1.1 bilioni vilivyotolewa na Taasisi ya Second Wind Foundation of Seabrook ya Texas, Marekani kwa kushirikiana na Kampuni ya Sakyambo Enterprise Company Limited ya Tanzania kwa lengo la kuboresha elimu.

Akizungumza baada ya kupokea vitabu hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rungwe, Renatus Mchau alisema Halmashauri ilikuwa na upungufu wa vitabu kwenye maktaba za shule hasa vya sayansi, hivyo vitasaidia wanafunzi kusoma kwa nafasi na kujiongezea maarifa zaidi.

“Tunamshukuru mdau huyu kwa kutukumbuka tulikuwa na upungufu mkubwa ila tunamuomba wakati mwingine atusaidie vitabu vya sayansi maana ndio eneo lenye upungufu mkubwa,” .

Mwakilishi wa Taasisi ya Second Wind Foundation of Seabrook, Clement Kilembe alisema wamelenga kuisaidia jamii katika sekta ya elimu na mpaka sasa wilaya saba zimeshanufaika na msaada wa vitabu kutoka kwao.

“Tunafikiria kuwekeza kwenye kilimo ili tupanue wigo wa kutoa ajira kwa jamii”alisema Kilembe.

Advertisement

Chanzo: www.mwananchi.co.tz