Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rotary Dar yagawa madaftari 600 kwa Shule ya Msingi Mbuyuni

905d2090c298278a3a1212a0fd631459 Rotary Dar yagawa madaftari 600 kwa Shule ya Msingi Mbuyuni

Thu, 17 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Wanachama wa Klabu ya Rotary ya jijini Dar es Salaam wamegawa madaftari 600 kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni iliyopo Oysterbay Ili kuwasaidia katika masomo yao.

Wanachama na wanafunzi hao walikutana mwishoni kwa wiki iliyopita ambapo walitumia muda wao mwingi kufurahi, kucheza na kujifunza pamoja na kuongeza maarifa na kuelimishana.

Akizungumza baada ya kugawa msaada huo Rais mteule wa Klabu hiyo, Deborah Da Silva alisema wamemua kutoa msaada huo Wanafunzi wa Shule ya msingi kwasababu ndiyo msingi wa elimu na ukuaji wa uchumi.

Alisema Septemba ni mwezi wa Elimu ya Msingi na Kusoma na katika kusherehekea mwezi huu , wanachama wa Klabu waliamua kukutana na wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Mbuyuni kwasababu eneo hilo ni karibu na kitovu au Ofisi Kuu ya Klabu hiyo.

“Shule ya Mbuyuni iko karibu na moyo wa klabu yetu , ilikuwa katika shule hii ambapo klabu yetu ilizindua mradi wetu wa kwanza wa elimu, mwaka 2019 tulifanya juhudi nyingi kutafuta fedha ili wanafunzi wa shule wapate maji safi ya kunywa.

“ Mnamo Januari, 2020, tulipata msaada wa kutoka Klabu ya Rotary ya Hereford kutoka Uingereza, shule hii ilipewa pampu mpya kabisa ya kuchuja maji, tuliwapatia pia vitabu kwa ajili ya chumba kipya cha maktaba ambacho kilikuwa kinahitajika sana,” alisema Deborah.

Kwa upande wake Rais aliyemaliza muda wake, Farhat Lane akizungumzia Elimu ya Msingi ilivyo muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa nchi alisema kujua kusoma na kuandika ni jambo muhimu kwa mafanikio ya mtu binafsi na ya jamii pia.

“Umri wa mwanzoni wa mtoto ni msingi wa ukuaji wa baadaye na msingi mzuri wa ujifunzaji wa maisha yote, maendeleo ya utambuzi na kijamii,” alisema Lane.

Aidha Lane alisema Klabu za Rotary zina maeneo saba wanayoyalenga ambayo ni pamoja na Elimu ya Msingi na kusoma na kuandika, Amani na Kuzuia Migogoro na Utatuzi, Kinga na Tiba ya Magonjwa, Maji na Usafi wa Mazingira, Afya ya Mama na Mtoto, Maendeleo ya Uchumi na Jamii na Mazingira.

“Kwa kuzingatia hayo Klabu yetu hufanya kazi kwa bidii kusaidia jamii zetu katika maeneo haya ya huduma na wanachama wa kilabu ambao wameundwa na wataalamu na marafiki wanaotaka kuleta mabadiliko Chanda katika jamii tunayoishi.

“Shughuli zetu za kutafuta fedha hufafanua jinsi tunavyoendesha klabu yetu, tunaangalia kila wakati kuleta raha na furaha katikhafla zetu zote, kusaidia jamii yetu na tabasamu,” alisema Lane.

Chanzo: habarileo.co.tz