Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rombo yafurika, LATRA yatoa vibali vya muda

Rombooo068346 Rombo yafurika, LATRA yatoa vibali vya muda

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) mkoa wa Kilimanjaro, imelazimika kutoa kibali kwa mabasi madogo ya abiria maarufu kama Coaster  ya  kukodi “special hire” ili kubeba abiria kuelekea wilaya ya Rombo kutokana na wingi wa abiria.

Wingi huo wa abiria unatakwa kusababisha uhaba mkubwa wa usafiri kwenye njia  hiyo janq Jumapili. Anaripoti Safina Sarwatt, Kilimanjaro…(endelea).

Mamlaka hiyo ilifanya ukaguzi kwa njia zote na kuelekeza mabasi kutoa kibali kwenye  njia zenye uhitaji wa abiria wengi na kuchukua hatua kwa gari za ruti kuzidisha nauli na kuvunja sheria ya usafirishaji.

Akizungumzia adha hiyo kwa waandishi wa habari Afisa mfawidhi mamlaka ya udhibithi usafiri ardhini LATRA mkoa wa Kilimanjaro, Paul Nyello amesema katika kipindi hiki cha sikukuu ya krimasi kuanzia tarehe 23-24 Desemba, abiria ni wengi na magari hayatosheleza mahitaji.

” Tarehe 23 na 24 abiria walizidi kushinda uwezo wa mabasi ya njia za Rombo na Tarakea ambapo ndipo kuna abiria wengi zaidi hali iliyolazimu mamlaka kuchukua hatua kwa magari makubwa kama coaster za kukodi maarufu special hire  na kupatana bei nafuu kwa abiria ,”amesema Nyello

“Mabasi makubwa ya masafa marefu kama Ngasere yalitoa huduma  pia,”

Amesema kuwa magari ya kukodi special hire yalitakiwa kuwabeba abiria katika njia hiyo kwa bei ya kupatana kwani yale magari yanasheria zake na utaratibu hasa ikizingatiwa yapo kwa ajili ya kukodiwa.

Amesema mamlaka ikishirikiana na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani walikuwa stendi na kuhakikisha abiria wote wanapata usafiri.

Amesema kuwa mamlaka hiyo pia ilifanya ukaguzi kwenye magari yote ya ruti za ndani na kuhoji abiria kama wamezidishiwa nauli lakini hakukuwa na abiria yoyote aliyelalamika.

Nao baadhi ya abiria wakizungumza kwa nyakati tofauti na wandishi wa habari wameshukuru LATRA kwa kusimamia vema suala la nauli na kuwasaidia kuwapatia usafiri kutokana magari katika njia Rombo Tarakea kutosheleza mahitaji yote ya abiria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live