Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rc aridhishwa kasi ujenzi vyumba madarasa Kahama

WhatsApp Image 2021 11 09 At 7.10.45 AM.jpeg Rc aridhishwa kasi ujenzi vyumba madarasa Kahama

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema ameeleza kuridhishwa na kazi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Wilayani Kahama.

Mjema amebainisha hayo leo ,alipokuwa kwenye ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Msalala, na Manispaa ya Kahama.

Amesema katika Halmashauri zote ambazo amepita kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa nyingi zipo kwenye hatua za msingi, lakini katika wilaya hiyo ya Kahama, jenzi  zipo kwenye hatua za upandishaji wa maboma, Renta na upauaji.

"Wilaya ya Kahama kasi yenu ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ni nzuri sana nimeipenda, na muendelee na kasi hiyo hiyo, na kukabidhi madarasa Novemba 20 hadi 28 kama mlivyoniahidi," amesema Mjema.

"Nataka katika mkoa wa Shinyanga tuwe wa kwanza kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa," amesema Mjema.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, amesema wilayani humo wamepokea fedha za ujenzi wa vyumba vya Madarasa Sh.bilioni 5.5 ambapo wanajenga Madarasa 247, na yote yapo katika hatua nzuri za ukamilishaji.

Chanzo: ippmedia.com