Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rangi nne zatawala msiba wa ndugu wanne waliokufa ajalini

IMG 20230808 WA0005 Rangi nne zatawala msiba wa ndugu wanne waliokufa ajalini

Tue, 8 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni msiba uliopambwa na rangi nyeusi, zambarau, nyeupe na nyekundu, hivi ndivyo inavyoweza kuelezwa kwa kile kinachoendelea kwenye msiba wa ndugu watatu.

Ndugu hawa Dk Norah, Sia na Diana walipata ajali usiku wa Agosti 2 sambamba na kaka yao Neech Msuya na wote kupoteza maisha.

Neech ambaye ndiye alikuwua kaka pekee wa familia hiyo alizikwa Agosti 6 kijijini kwao Msangeni Ugweno wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Leo Agosti 8 ndiyo siku ndugu waliosalia watazikwa katika makaburi ya Kondo baada ya kuagwa katika viwanja vya gofu Kawe jijini Dar es Salaam.

Tayari mamia ya waombolezaji wamewasili katika viwanja hivi wakisubiri kuanza kwa ibada na hatimaye shughuli ya kuwaaga wanafamilia hawa kabla ya kuwasindikiza katika safari yao ya mwisho.

Kama ilivyo ada mambo yanayowagusa wanawake kuwa na taswira ya aina yake, wanawake wengi waliojitokeza hapa wanamuonekano wa kufanana.

Mavazi meusi ni kawaida kuonekana msibani ila leo wanawake wamejiongeza na kuvaa vikofia vya rangi ya zambarau na wengine wamevaa vya rangi nyekundu.

Wasio na vikofia hivyo wametupia skafu za rangi hizo hizo au mitandio ya rangi nyeupe na hii ndiyo maana sahihi ya rangi hizi nne kutawala kwenye msiba huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live