Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais atoa ndege kwa Mawaziri kutatua changamoto ya Miundombinu Lindi

Ndege Jeshii Rais atoa ndege kwa Mawaziri kutatua changamoto ya Miundombinu Lindi

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Helikopta kwa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Deo Ndejembi kufika Wilaya ya Liwale kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya miundombinu ya barabara na madaraja kutokana na mvua kubwa kunyesha na kusababisha barabara kufungwa.

Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Helikopta kwa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Deo Ndejembi kufika Wilaya ya Liwale kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya miundombinu ya barabara na madaraja kutokana na mvua kubwa kunyesha na kusababisha barabara kufungwa. Mawaziri hao wamewasili Wilayani Liwale Mkoani Lindi leo March 05, 2024 wakiwa wameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack na Wataalam kutoka Wakala ya Barabara (TANROADS) na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya miundombinu ya barabara na madaraja yanayounganisha Wilaya hiyo na sehemu nyingine kujaa maji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live