Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia mgeni rasmi Tamasha la Utamaduni Kilimanjaro

008fb9ea4a43422e610e0368c9cca5d9 Rais Samia

Sun, 9 Jan 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Utamaduni la Mkoa wa Kilimanjaro litakalofanyika Januari 22, 2022 Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Manispaa ya Moshi.

Taarifa hiyo imetolewa na Umoja wa Machifu wa mkoa huo chini ya Mkuu wa Chifu nchini ambaye ni Mkuu wa Chifu wa Mkoa wa Kilimanjaro Chifu Frank Mareale wa himaya ya Marangu katika katika kikao cha Machifu wa mkoa huo kilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.

“Ni heshima mkoa wetu kuwa wa kwanza kutekeleza agizo la Chifu Mkuu Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambalo alilitoa mkoani Mwanza tarehe 8 Septemba 2021 katika Tamasha la Utamaduni ambalo aliagiza mikoa yote nchini kuendesha matamasha ya utamaduni kwa lengo la kuelimisha jamii na kuendeleza utamaduni wetu” amesema Chifu Mareale.

Chanzo: www.habarileo.co.tz