Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia kupokea na kuzindua Rasmi Chuo cha VETA Kagera

IMG 20221012 WA0006 Rais Samia kupokea na kuzindua Rasmi Chuo cha VETA Kagera

Thu, 13 Oct 2022 Chanzo: Global Publishers

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania anatarajia kupokea na kuzindua Chuo kipya cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) cha Mkoa wa Kagera.

Halfa hiyo inatarajiwa kufanyika Alhamisi Oktoba 14, 2022. Katika Chuo hicho kipya kilichopo Burugo Nyakato Kagera.

Chuu hicho chenye karakana, vifaa na miundo mbinu ya kisasa kimejengwa kwa msaada wa Sefikali ya China kitakuwa na uwezo wa kuchikha wanafunzi zaidi ya 1,400 kwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu katika fani mbalimbali za ufundi na huduma.

Hayo yameelezwa na Prof. Adolf Mkenda Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipokagua maandilizi ya halfa hiyo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wa Nyakato, kagera na mikoa mingine kushiriki katika ufunguzi.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea fursa mbalimbali za mafunzo zitokanazo na uwepo wa Chuo hicho na kuwataka vijana kujiunga na mafunzo ambayo yanalenga katika kujenga ujuzi.

Chanzo: Global Publishers