Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia awaapisha Mchengerwa na Pindi Chana

Chana Mchengerwa D.jpeg Rais Samia awaapisha Mchengerwa na Pindi Chana

Thu, 16 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk Hassan Abbasi wametakiwa kuepuka vishawishi vya uuzwaji wa vitalu, huku Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pinda Chana akitakiwa kuepuka migogoro isiyo na tija kwa wasaidizi wake.

Akizungumza mara baada ya uapisho wa mawaziri hao jana Februari 15, 2023 Ikulu jijini Dar e Salaam, Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amesema Wizara ya Mali asili inaongoza kwa kupita mawaziri wengi zaidi kwa vile imejaa vishawishi.

“Wizara ya Maliasili historia kidogo ina mafunzo mengi, kati ya wizara ya inayoongoza kupita mawaziri wengi ni maliasili, ni sekta ambayo mchango wake fedha za kigeni, ajira ni kubwa sana, umepewa dhamana kubwa kuhakikisha sekta inakuwa na kuchangia zaidi katika maendeleo ya nchi yetu.

“Sekta hiyo bahati mbaya ina vishawishi vingi, naamini Pindi Chana atakueleza katika kipindi kifupi alichokaa hapo vishawishi alivyokutana navyo. Nadhani mjiepushe na vishawishi hivyo, kwenye vitalu na mengineo, ”amesisitiza Dk Mpango.

Kwa upande wa Wizara ya Utamaduni, Dk Mpango amesema ni sekta kwenye takwimu inaonesha kukua kuliko sekta zote na inaajiri vijana wengi tegemeo la kesho na kumtaka Waziri Pindi Chana kuitendea haki wizara hiyo, kwani vijana wanaitegemea sana sekta hiyo.



“Moja ninaloweza kusema ni mashirikiano kati yako na wasaidizi wako, bado tunaona changamoto katika wizara mbalimbali, tumezungumza mara kadhaa, Rais amelieleza, mivutano kati ya Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Waziri haina tija, mkae kama timu moja mfanye kazi katika sekta mtakazoenda kuziongoza,”amesema.

Dkt Mpango amempongeza Rais Samia kwa kufanya mabadiliko kwa mawaziri hao kwa kumpeleka Mchengerwa Maliasili na Utalii, huku Pindi Chana akitolewa wizara hiyo na kupelekwa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.

“Kocha yoyote anangalia timu yake inavyocheza, anaangalia abadilishe huyu kwenda ‘defense’ huyu kwenda huku mradi timu ifunge magoli….; “Mmebadilishana namba naamini jambo la kwanza mtakalofanya ni kubadilishana uzoefu, changamoto ni zipi, mkazifanyie kazi,” amesema Dk Mpango.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live