Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia amwaga sh bilioni 351 Kagera

Rais Samia Chato 8 Rais Samia akizungumza na wananchi

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbughe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka kiasi cha shilingi Bilioni 351 mkoani humo ambazo ni fedha za maendeleo kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi Februari 2022.

RC Mbughe ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT amemsifia Rais Samia kwa ubunifu wake katika uandaaji wa Filamu ya The Royal Tour ambayo kimsingi hadi sasa umechangia kuvutia idadi kubwa ya watalii nchini.

RC Jenerali Mbughe amesema kwa upande wa madarasa Mkoa wa Kagera umefanikiwa kujenga idadi ya madarasa 881 ambapo katika Wilaya ya Biharamuro pekeyake yamejengwa madarasa 159 na kuhakikisha hakuna Shule ambayo imekosa madarasa.

Akitoa ripoti kwa Rais Samia kuhusu hali ya Uviko-19 ndani ya Mkoa huo Meja Jenerali Mbughe amesema Elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi kuhusu kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo lakini kubwa zaidi ni kwamba wananchi wanaendelea kupata chanjo kama kawaida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live