Geita. Rais wa Tanzania, John Magufuli ametuma salamu za pole kwa ndugu na jamaa ambao bado wapendwa wao ambao ni wachimbaji wawili wapo chini ya ardhi kwa siku tatu sasa.
Akizungumza na ndugu pamoja na wananchi waliopo eneo la machimbo ya Imalanguzu kata ya Lwamgasa Wilaya na Mkoa wa Geita leo Alhamisi Oktoba 3, 2019 Waziri wa Madini nchini Tanzania, Doto Biteko amesema Rasi Magufuli ametoa pole na kuwataka wananchi waendelee kuwaombea ili waokolewe wakiwa salama.
Amesema kwa sasa sio muda wa kulaumu au kutafuta mchawi kwani juhudi kubwa zinazofanyika sasa ni kuona namna ya kuwaokoa wachimbaji hao wakiwa hai.
Mke wa mmoja wa wachimbaji waliofukiwa Jenipha Malimi amesema mume wake Septemba 30, 2019 aliaga anakwenda kazini lakini alikua akisita.
Jenipha alisema mme wake huyo wakati anakwenda alisema hakuwa anajisikia kwenda kazini na saa 12 jioni ndio aliamua kuondoka hivyo hivyo na siku iliyofuata alfajiri alipokea simu kutoka kwa rafiki wa mume wake akieleza mumewe amefukiwa na kifusi cha udongo.
Pia Soma
- Vigogo polisi kizimbani kwa madai ya kuomba rushwa ya Sh200 milioni
- Majaliwa amjibu kwa vitendo Mizengo Pinda
- Wavua tani moja ya pweza kwa siku tatu