Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi vifo vya watu 15 Mbeya

16289 Rambi+pic TanzaniaWeb

Sun, 9 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi baada ya watu zaidi ya 11 kupoteza maisha katika ajali ya barabarani  mlima wa Igawilo, Mbeya jana Septemba 7.

Hata hivyo Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Petro Seme amesema watu 15 wamefariki dunia mpaka sasa kutokana na ajali hiyo.

 Akituma salamu hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, Rais Magufuli amesema;

“Nimepokea kwa mshtuko taarifa ya vifo vya watu 11 vilivyotokea leo jioni huko Mbeya, kwa mara nyingine tumewapoteza Watanzania wenzetu katika ajali ya barabarani na wengine wameumia, nimesitishwa sana na vifo hivi.

“Nawapa pole wanafamilia wote waliopoteza ndugu zao katika ajali hii na pia nawapa pole majeruhi wote, nawaombea watibiwe na kupona haraka ili waweze kuungana na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku.”

Ajali hiyo imetokea  jana Septemba 7 2018 majira ya saa 10 jioni katika mteremko wa mlima wa Igawilo Jijini Mbeya baada ya Lori lililokuwa na shehena ya viazi, likitokea Tukuyu kwenda Mbeya Mjini kuyagonga magari matano likiwemo basi dogo lililokuwa na abiria.

Pamoja na kutoa pole kwa wafiwa wote, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na vifo hivyo Rais Magufuli amewaombea Marehemu wote wapumzike mahali pema peponi.

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz