Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Radi yaua wavuvi Mtwara

Radi Yaua Wachezaji Wa Soka Magharibi Mwa Kenya Radi yaua wavuvi Mtwara

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wavuvi wawili ambao ni Ndugu, Shani Salum Yusuph (53) na Nangomwa Salum Yusuph (58), Wakazi wa Kijiji cha Mtandi Mkoani Mtwara wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi wakati wakiendelea na uvuvi jana March 19,2023 katika Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Msimbati Mkoani Mtwara.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amenukuliwa akisema “Jana majira ya asubuhi Wavuvi hao ambao ni Ndugu walienda katika shughuli za uvuvi wa samaki katika Bahari ya Hindi wakiwa na Mtumbwi usio na usajili ambao ni mali yao, wakiwa wanaendelea na shughuli za uvuvi, mvua kubwa ilianza kunyesha na ndipo ghafla walipopigwa na radi na kufariki dunia”

“Tukio hilo lilishuhudiwa na Wavuvi wenzao waliokuwa maeneo ya jirani na tukio na ndipo walipotoa taarifa Kituo cha Polisi ambapo juhudi zilifanyika kufikisha miili ufukweni”

“Uchunguzi wa mili ya Marehemu uliofanywa na Daktari umebaini kuwa sababu ya vifo hivyo ni kupigwa na radi”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live