Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Radi yaua mtoto Arumeru, sita wajeruhiwa

85627 Pic+radi Radi yaua mtoto Arumeru, sita wajeruhiwa

Sun, 24 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mtoto Mejoole Loitale (14) mkazi wa kata ya Sambasha, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha amefariki dunia jana jioni Jumamosi Novemba 23, 2019 kwa kupigwa na radi huku watu wengine sita wakijeruhiwa.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amesema jana jioni ilinyesha mvua iliyoambatana na radi ambapo katika kata ya Sambasha wilaya ya Arumeru radi ilipiga na kusababisha madhara kwa watu sita na mmoja kufariki.

Muro amesema Loitale alifariki wakati jitihada za kumkimbiza hospital zikifanyika na majeruhi mmoja amelazwa Hospitali ya Seliani Ngaramtoni Melau likindasaru loita( 35) huku wengine watatu wamerudi nyumbani kutokana na kutopata madhara makubwa.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa rai kwa wananchi wote wa Arumeru kuendelea kuchukua tahadhari wakati wa kipindi hiki cha mvua kikiendelea kwa kuhakikisha hawakai chini ya miti au kwenye nguzo za nyaya za umeme.

"Natoa pole kwa familia ya marehemu na kuendelea kuwaombea majeruhi wapone haraka na kurejea katika shughuli zao za kawaida za kijamii," amesema

Muro ameeleza kuwa nyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na vikosi vya zimamoto na uokoaji viko katika hali ya tahadhari na utayari wa kukabiliana na majanga

Chanzo: mwananchi.co.tz