Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Radi yaua mmoja Kaliua

53655 Pic+radi

Tue, 23 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Mkazi wa kijiji cha Ulindwanoni, wilayani Kaliua, Saada Athuman, amefariki dunia baada ya kupigwa radi akiwa nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema tukio hilo, limetokea siku ya Pasaka usiku wakati ambao mvua ilikuwa ikinyesha.

Kamanda Nley ametaka wananchi kuchukua tahadhari wakati mvua na radi inapokuwepo ili kuepusha madhara .

Mume wa marehemu Abubakar Saleh, amesema walikuwa ndani mkewe ambaye baadaye alimuomba amshikie mtoto ili aende nje kutoa vyombo kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.

“Baada ya muda mtoto wao mwingine aliyekuwa na mama yake aliingia ndani na kusema amepigwa radi na mama yake ameanguka,” amesema Saleh.

Amesema walimbeba wakamuingiza ndani na kuanza kumpepea lakini baadhi ya watu waliokuwapo walitaka apelekwe kituo cha afya na baada ya kufika katika kituo cha afya vipimo vilionyesha alikuwa tayari amefariki.

Katibu tawala wa wilaya ya Kaliua, Michael Nyahinga akitoa pole kwa niaba ya Serikali, amesema wamesikitishwa kwa kumpoteza raia mwema huku akiwahimiza wananchi kuchukua tahadhari kwa kutoka kwenye miti pindi mvua inaponyesha ili kuepuka majanga ya kupigwa radi.



Chanzo: mwananchi.co.tz