Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Radi yageuza sherehe kuwa msiba Mtwara

Radi Yaua Wachezaji Wa Soka Magharibi Mwa Kenya Radi yageuza sherehe kuwa msiba Mtwara

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtwara. Watu sita wamefariki dunia na watano wamejeruhiwa kwa kupigwa na radi wakiwa katika sherehe za kumpongeza kijana aliyemaliza kidato cha nne.

Tukio hilo limetokea jana Desemba 3, 2023 majira ya saa 12 jioni katika Kijiji cha Maparagwe Kata ya Chikukwe Wilaya ya Masasi.

Watu hao walikutwa na maafa hayo wakiwa kwenye sherehe ya kumpongeza kijana wao aliyehitimu kidato cha nne nyumbani kwao, ambapo mvua ilianza kunyesha ikiambatana na radi.

Akielezea mkasa huo, shuhuda wa tukio hilo, Suzana Bakari mkazi wa Kijiji cha Maparagwe amesema siku ya jana walikuwa kwenye shughuli ya mahafali ya kijana wa kidato cha nne pamoja na mtoto aliyekuwa ametoka jandoni mwenye umri wa miaka minane.

“Ilikuwa ni sherehe kubwa, tulikuwa watu wengi kama unavyojua sherehe yenye muziki. Ulipofika muda wa kufupa (kutoa zawadi) hapo ndipo yalianza manyunyu ambayo yaliondoa watu wengi katika eneo hilo na baadhi walienda kukaa chini ya mti na wengine majumbani. Mimi nilipoona mvua nilikimbilia kwenye nyumba ya jirani nikakaa,” anasema Bakari.

“Mara nikasikia radi kubwa sana ambayo iliacha maswali kwa wengi, baada ya hali kutulia ndipo tulibaini kuwa kuna wenzetu waliokuwa chini ya mti wamelala, tulisongwa kwa kweli tulishtuka na tukaenda kuwasaidia na kuwawahisha hospitalini ” amesema Bakari.

“Sherehe ndio ilikuwa katikati, yaani tulikuwa tunamaliza kutoa zawadi kisha tule. Ile shughuli haikuwisha wala hakikuliwa kitu, ilikuwa ni simanzi na sasa tuko kwenye misiba zaidi ya sita ya majirani na nyumba iliyokuwa ikifanya sherehe,” amesema Bakari.

Frank Maurusu (ndugu wa Marehemu) amesema baada ya kunyesha ilipiga radi iliyoondoka na maisha ya watu, akiwemo mdogo wake.

“Muziki ulikuwa unapiga na mvua ilikuwa inanyesha, sio kubwa sana lakini ilipiga radi kubwa iliyosababisha muziki kuleta shida, mara ya tatu tumestuka wenzetu wako chini. Tulilazimika kuwasaidia katika tukio hilo, mtu mmoja alifariki palepale ambaye nia ndugu yangu Patrick Said Maurus,” amesema Frank.

Naye Unika Malilo aliyekuwa msherekeshaji wa shughuli hiyo, amesema, “yalikuwa ni mahafali na unyago, sherehe ilikuwa ya kawaida hata hali ya hewa ilikuwa nzuri lakini katikati ya shughuli hali ilibadilika ikanyesha mvua. Tukasubiri mvua imalizike na baadhi walikaa kwenye majumba ya wengine chini ya mikorosho miwili.

“Radi ilipiga mara tatu, wote tukatararuki na wengine walitawanyika, baadaye naangalia kwenye miti nikaona watu wakiwa wamelala chini, kumbe walijeruhiwa na ile radi na kwa haraka tuliwapeleka hospitalini, lakini mpaka sasa tuna misiba saba” amesema Malilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Desemba 04, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Nikodemus Katembo amewataja waliofariki kuwa ni Patrick Said Maurus (42), Fatuma Rashid (40) Rosina Wales (46), Regina Vincent (55), Zainab Abdulahman (62), Zainab Mussa (44).

Amewataja majeruhi kuwa ni Amina Abdulahman (62), Haiman Fadhili (4), John Nguli (39), Luiz William (39) Mzamiru Said (2).

Amesema baada ya tukio hilo majeruhi walifikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Benedict, Ndanda iliyopo Masasi na wanaendelea matibabu na milii ya marehemu imefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kukabidhiwa kwa ndugu.

Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Lauther Kanoni amesema kKwa sasa tufanya taratibu za maziko ambapo wote ambao ni majirani tutawazika leo, tumeweka misiba kulingana na dini zao na tumegharamia taratibu za mazishi na tunawahudumia waliopo hospitali.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live