Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Radi, ajali zaua wanafunzi sita

E82e826231c85e395fd5e6b6ea5aceb4 Radi, ajali zaua wanafunzi sita

Sat, 20 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WANAFUNZI sita wakiwamo watatu wa familia moja wa shule tofauti za msingi katika Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa wamepoteza maisha wanne kwa kupigwa na radi na kugongwa na gari.

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda, amethibitisha kuwapo kwa vifo hivyo na kusema watoto hao walipoteza maisha juzi jioni wanne kwa kupigwa na radi huku wawili wakifariki baada ya kugongwa na gari.

Aliwataja watoto watatu wa familia moja waliopoteza maisha baada ya kupigwa na radi kuwa ni Rita Chiwile (6) aliyekuwa akisoma darasa la awali katika Shule ya Msingi Nkana, Macrida Mtepa (7) alikuwa darasa la kwanza na Exavery Chipamba (13) aliyekuwa akisoma darasa la sita.

Mwingine ambaye si miongoni mwa watoto wa familia hiyo ni Kwilasa Siri (9) aliyekuwa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Ncheje na alipigwa na radi akiwa nyumbani kwao. Waliopoteza maisha kutokana na kugongwa na gari wametambuliwa kuwa ni pamoja na Boniface Sapi (8) aliyekuwa darasa la pili katika Shule ya Msingi Kipundukala na Debora Chulula (12) aliyekuwa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Chala.

Akizungumza na HabariLeo, Ofisa Elimu Wilaya ya Nkasi, Agnes Martin alisema jioni ya siku hiyo ya tukio, watoto hao marehemu wa familia moja walikuwa wakicheza michezo ya kitoto na wenzao kumi na moja ambao hawakujeruhiwa baada ya radi kupiga.

Chanzo: habarileo.co.tz