Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RUWASA yahimiziwa ushirikiano na Halmashauri

4034f0d21594cfac8e5f832d5c98b1b2 RUWASA yahimiziwa ushirikiano na Halmashauri

Tue, 13 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAOFISA wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wametakiwa kuhakikisha wanakuwa na uhusiano mzuri na Halmashauri za miji,mikoa na wilaya kwa lengo la kuhakikisha wanashirikiana vyema katika kutatua kero za Maji kwa wananchi.

Rai hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa bodi ya wakala wa maji na usafi vijijini(RUWASA) ,Profesa Idrissa Mshoro wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wadau wa mamlaka hiyo kutoka mikoa ya Mwanza,Mara,Geita,Pwani na Simiyu.

Profesa Mshoro alisema kumekuwa na changamoto kubwa sana Halmashauri hazipati taarifa za Ruwasa kama wanavyotarajia.

Alisema Ruwasa inatakiwa kupeleka ripoti zao katika mikoa na wilayani. Profesa Mshoro ni muhimu viongozi wakaonyesha njia kwa kudumisha dhana ya ushirikiano katika ngazi ya mipango, bajeti na mawasiliano

Alisema watumie fursa ya mtazamo, msimamo na msisitizo wa wizara ya maji katika ufanyaji kazi kama wizara moja.

Profesa Mshoro alisema Ruwasa inatakiwa kuongeza tija ya utoaji huduma ya maji vijijini. Alisema mamlaka yao imewekeza nguvu sana katika utekelezaji miradi kuliko utoaji huduma.

Kaimu Mkurugenzi mkuu wa RUWASA,Mhandisi Mkama Bwire alisema ndani ya mwaka moja bodi yao imetumia nguvu nyingi sana katika ukamilishaji wa miradi kuliko katika utoaji wa huduma.

Alisema bado upatikanaji wa maji katika maeneo ya vijijini sio ya kuridhisha. Alisema mamlaka yao inahaja kubwa sana ya kuhakikisha inaweka mskumo katika utoaji huduma.

Chanzo: habarileo.co.tz