Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RPC kizimbani kutoa ushahidi kesi ya ‘unga’

9470 PIC+RPC TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mahakama Kuu Kanda ya Moshi imemuona raia wa Kenya, Josephine Mumbi Waithera kuwa ana kesi ya kujibu katika shtaka la kusafirisha dawa za kulevya kwenda Vienna nchini Austria.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Patricia Fikirini, baada ya upande wa mashtaka katika kesi hiyo kufunga ushahidi wakimalizia na kamanda wa polisi mkoani Arusha, Ramadhan Ng’anzi.

Ng’anzi, ndiye aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa makosa ya Jinai (RCO) mkoa wa Kilimanjaro wakati mshtakiwa anakamatwa 2012.

Katika uamuzi wake huo, Jaji Fikirini alisema kutokana na ushahidi wa mashahidi sita na vielelezo vinane vya upande wa mashtaka, amemuona mshtakiwa ana kesi ya kujibu hivyo atatakiwa kujitetea.

Mshitakiwa huyo alipangiwa kuanza kujitetea jana hiyohiyo saa 8:00 mchana akiongozwa na wakili wake, Ralph Njau. Mwaka 2016, Josephine alihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia katika kosa hilo lakini Mahakama ya Rufaa ikaamuru kesi isikilizwe upya.

Chanzo: mwananchi.co.tz