Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RPC Moro awaaga askari, awaachia ujumbe wa rushwa

76747 Pic+mutafungwa

Sun, 22 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro (RPC) Wilbroad Mutafungwa amesema atahakikisha jeshi la polisi linaendelea kuheshimika, kuaminika machoni mwa wananchi pamoja na kutegemewa.

Kamanda huyo amesema hayo leo Jumapili Septemba 22,2019 wakati akiwaaga askari wa jeshi hilo na waandishi wa habari mkoa humo.

Septemba 17, 2019 Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro alitangaza mabadiliko ya makamanda wa polisi wa baadhi ya mikoa ambapo Mutafungwa amehamishiwa makao makuu ya polisi na nafasi yake kuchukuliwa na Hamisi Issa aliyekuwa Kilimanjaro. 

Mutafungwa amesema pamoja na kuondoka mkoani humo amewaasa askari hao kuendelea kufanya kazi kwa weledi, kuachana na vitendo vya rushwa kwani imekuwa ikichafua taswira ya jeshi la polisi.

Amewataka kuendelea kufanya kazi zao kwa kufuata sheria na miongozo iliyowekwa na jeshi hilo.

Amesema katika kuendelea kutekeleza majukumu yao askari hao wawe na ushirikiano na taasisi nyingine katika kuendelea kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji pamoja na migogoro ya ardhi ambayo alieleza kwa kiasi kikubwa askari hao wameweza kushiriki kikamilifu katika kuondoa migogoro hiyo.

Pia Soma

Advertisement
“Kuna changamoto ya usalama barabarani hasa ajari, unyang’anyi wa kutumia silaha na matukio ya wizi na utekaji magari hapa, kuna wale watu wanaitwa shushashusha wamekuwa wakifanya vitendo hivyo ingawa katika wakati wangu vilionekana kupungua visije vikajirudia kwani magari mengi yamekuwa yakipita na mizigo ya watu kwenda nchi jirani na hii ni kutaka kuiweka taswira ya nchi na jeshi la polisi naomba muendelee kukaza uzi,” amesema Mutafungwa.

Pamoja na kuwaaga askari hao, amewashukuru wananchi na waandishi wa habari wa mkoa huo kwa namna walivyoonyesha ushirikiano wakati wote, lengo likiwa ni kuhakikisha mkoa unakuwa katika hali ya usalama na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano huo kwa kamanda anayekuja.

Chanzo: mwananchi.co.tz