Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RPC Kilimanjaro atoa masharti kusherehekea mwaka mpya

Kilimanjaro Pic Data RPC Kilimanjaro atoa masharti kusherehekea mwaka mpya

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limepiga marufuku ufyatuaji wa fataki na uchomaji wa matairi barabarani wakati wa kusherehekea Mwaka Mpya 2022 na kusema litawachukulia hatua kali wale wote watakaokiuka agizo hilo.   Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Desemba 31, 2021 Kamanda wa Polisi mkoani humo, Simon Maigwa amewataka wale wote wanaotaka kufyatua fataki usiku wa kuupokea mwaka mpaya waombe vibali ili kujua ni eneo gani haswa ambalo litafanya hivyo ili kuwapa tahadhari wananchi wa maeneo hayo.

"Tumejipanga mkoa mzima kuhakikisha wananchi wanasherekea kwa amani, kikubwa ambacho hatutaki wakati huu wa kuukaribisha mwaka mpya, tumezuia matukio ya watu kupiga fataki kwa kigezo kuwa wanasherekea sikukuu, tukimbaini tutamchukulia hatua,"amesema Kamanda Maiga na kuongeza

"Kama ni suala la kupiga fataki, watu waombee vibali ili tujue kwamba ni eneo flani linapiga fataki ili tuwaandae wananchi kwasababu tutashindwa kujua hii milipuko ni ya risasi au ni ya uhalifu kwa hiyo maeneo ya mipakani tumejipanga vya kutosha na hali itendele kuwa shwari niwaombe tuu wananchi waisherekee kwa amani siku hii ya mwaka mpya," alisema na kuongeza

"Ukiingia kwenye uvunjifu wa amani sisi tuko tayari kupambana na yeyote atakayevunja uvunjifu wa amani wakati huu wa mwaka mpya,hasa kwenye maeneo ya mpaka kama vile Holili,Tarakea na maeneo yote ambayo ni ya mpakani  ,"alisema Kamanda Maigwa

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga  amesema katika wilaya hiyo ambayo iko mpakani wataendelea kuhakikisha amani na utulivu vinatawala wakati huu wa mwaka mpya na kusema wamejipanga kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa salama.

Aidha alisema ziko mbinu ambazo wameziweka kukabiliana na matukio ya uhalifu kwenye maeneo hayo  na kutoa angalizo kwa wale ambao wamepanga kufanya vurugu wakati huu wa sikukuu za mwaka mpya.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz