Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RPC Arusha ahamasisha uandikishaji Serikali za mitaa

80002 PIC+ARUSHA

Tue, 15 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kupata fursa kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu Oktoba 14, 2019 na kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana baada ya kutembelea vituo vya kujiandikisha wapiga kura.

Amesema polisi wameimarisha usalama kuwawezesha wananchi kujiandikisha kwa amani na utulivu.

"Nimekuta uandikishaji umedorora natoa wito kwa wananchi kutumia siku tatu zilizoongezwa ili wajiandikishe kwa wingi,” amesema.

“Tutatumia mwongozo wa  uchaguzi wa Serikali za mitaa, sheria na taratibu za polisi zilizopo katika mwongozo wa jeshi wakati wote wa kampeni, kupiga kura hadi kutangazwa matokeo.”

Amesema wasimamizi wa uchaguzi kwenye halmashauri zote za wilaya mkoani humo watawasilisha miongozo, kanuni  na taratibu za uchaguzi kwa wakuu wa polisi wa Wilaya .

Pia Soma

Advertisement
Watu milioni 1.9 wanatarajiwa kuandikishwa na hadi sasa waliojiandikisha hawajaika nusu ya idadi hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz