Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC azionya taasisi zinazokataa vyeti vya kuzaliwa

HOMERA RC azionya taasisi zinazokataa vyeti vya kuzaliwa

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amezitaka taasisi za umma na binafsi Mkoani Mbeya, kuacha tabia ya kukataa kupokea vyeti vya kuzaliwa, vinavyo andikwa kwa mkono na wasajili wasaidizi katika vituo vya kutolea huduma za afya, kwa madai kwamba ni tangazo na sio vyeti halisi.

Homera ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mbeya, katika uzinduzi wa kampeni ya utoaji wa vyeti hivyo kwa watoto walio chini ya miaka 5, ambapo takwimu zinaonyesha watoto zaidi ya elfu 60 hawaja chukua vyeti kati ya watoto zaidi ya elfu 80 waliozaliwa hai kwa mwaka 2022.

Msajili wa RITA Wilaya ya Mbeya Veronica Mayombo, Amesema vyeti vyote vinavyo andikwa kwa Mkono na kutolewa na masajili msaidizi katika vituo vya kutolea huduma za afya ni halisi na havina ukomo wa muda Wala umri wa Mtoto kwakua vinatolewa na Mamlaka husika, huku baadhi ya wananchi wakiiomba serikali kuzungumza na taasisi zinazo kataa vyeti hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live