Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC awataka madiwani kuwa na shughuli mbadala za kipato

8347fd803d969accc34604e3b789f355 RC awataka madiwani kuwa na shughuli mbadala za kipato

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Dk Philemon Sengati amewataka madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nzega kuhakikisha wanakua na shughuli mbadala za kuwaingizia kipato na sio kutegemea nafasi ya udiwani kwa ajili kuendesha maisha yao.

Alisema madiwani watambue kuwa nafasi zao walichaguliwa na wananchi ni sawa na utumishi na sio ajira ni vema wakiwa na kazi halali ya kuwapatia kipato.

Dk Sengati alisema hayo wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa Baraza jipya la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.

“Watu wengi wanagombea nafasi ya udiwani wakiamini kuwa nafasi hiyo ni sehemu ya ajira...sharti madiwani muwe na shughuli nyingine za kujipatia kipato cha kuwasaidia kutatua matatizo yenu na kujiletea maendeleo,” alisisitiza.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema wanatakiwa kuchapakazi ikiwemo kutatua kero za wananchi na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Dk Sengati aliongeza kuwa wanatakiwa kutumia ukaribu wao na wananchi kusimamia rasilimali za umma ili ziweze kutumika kwa usahihi kwa ajili ya manufaa ya jamii zote anayoiongoza.

“Nyinyi viongozi na walinzi hakikisheni fedha na mali nyingine za halmashauri na mali nyingine zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ...michango yoyote inayotolewa na wananchi kwa ajili ya maendeleo yao lazima izae matunda kwa manufaa ya wananchi,” alisema.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa amewataka madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nzega kuhakikisha wanashirikiana na watendaji katika maeneo yao kukabiliana na upungufu wa madarasa na viti na meza.Alisema halmashauri hiyo inakabiliwa na upungufu wa madarasa 16, viti na meza 2,285.

Dk Sengati alisema watoto wote waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba na kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwakani wapatao 3,788 lazima wajiunge la Kidato cha Kwanza kabla ya mwezi Machi.

Chanzo: habarileo.co.tz