Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC awapa kazi nzito watendaji madarasa kidato cha kwanza

Fa5e0c6b0c9ccb525a97f0559eacdbe2.png RC awapa kazi nzito watendaji madarasa kidato cha kwanza

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira ameagiza watendaji ikiwemo wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha kuwa wanakamilisha ujenzi wa madarasa mkoani humo ili wanafunzi waliomaliza darasa la saba na kuchaguliwa wapate nafasi ya kuendelea na masomo.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa kuna wanafunzi 3,000 wamekosa nafasi kutokana na ukosefu wa vyumba vya madarasa.

Akizungumza na watendaji wa halmashauri, katika kikao maalumu cha kujadili changamoto ya uhaba wa madarasa,Mghwira alisema mkoa wa Kilimanjaro katika wilaya za Hai, Moshi Vijijini, Same na Siha wanakabiliwa na uhaba wa madarasa zaidi ya 60 na kuwa changamoto hiyo imesababisha wanafunzi hao kukosa nafasi ya kuendelea na kidato cha kwanza.

“Katika mwaka 2021 wa masomo wanafunzi 2900 hawataweza kuendelea na kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa madarasa, wilaya ya Hai ni wanafunzi 890, Moshi vijijini 350, Same 1,414 na Siha 350,” alisema na kuongeza kuwa wilaya ya Hai inakabiliwa na uhaba wa madarasa 18, Moshi Vijijini saba, Same 28 na Siha saba na kwamba halmashauri peke ambazo hazijakabiliwa na changamoto hizo ni pamoja na Moshi manispaa, Rombo na Mwanga.

Katika hatua nyingine ,Mkuu huyo wa mkoa alimuagiza Ofisa Elimu mkoa wa Kilimanjaro, Paulina Mkwama kuhakikisha anarekebisha Ikama ya walimu katika baadhi ya wilaya kutokana na kuwepo kwa upungufu mkubwa wa walimu na maeneo mengine kuzidi na kutokuwa na uwiano.

Ofisa Elimu mkoa wa Kilimanjaro, Paulina Mkwama alisema jumla ya wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani ni 34,900 na kwamba waliofanikiwa kufanya ni 34,744 huku wanafunzi 156 wakishindwa kufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro.

“Watahiniwa waliofaulu ni 30,834 na inaoneesha mjongeo chanya ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2019 ufaulu ulikuwa kwa asilimia 87.74 na mwaka huu nii asilimia 88.90,” alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Same, Annastazia Tutuba alisema ili kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa wamekubalina kila mkuu wa idara kuchanga kiasi cha Sh 50,000 kila moja na wikiwemo wakuu wote wa shule.

Chanzo: habarileo.co.tz