Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC awabana watendaji wa Mikumi

97cc6f9410666bae45d11c491f62522a RC awabana watendaji wa Mikumi

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare, amewapa siku 11 wenyeviti wa serikali za mitaa na viongozi wa mji mdogo wa Mikumi wilayani Kilosa kukamilisha ukusanyaji michango kwa ajili ya ujenzi vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Mikumi.

Sanare alitoa agizo hilo kwenye mkutano na viongozi wa serikali ya wilaya ya Kilosa na wa mji mdogo Mikumi na akaagiza kazi hiyo iishe ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Alitoa agizo hilo alipokuwa kwenye ziara kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa katika shule hiyo.

Sanare aliwataka viongozi hao wahakikishe kila mwananchi anayestahili kutoa mchango anachanga kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo kabla ya mwisho mwa mwezi huu vinginevyo sheria kali zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kutiwa mbaroni.

Aliwataka watendaji kutomuogopa mtu yeyote katika utendaji wao na akasisitiza kutoa taarifa kwa mamlaka husika iwapo kuna hali ya uvunjaji wa sheria za kazi.

Hata hivyo, alisema katika suala la mapato katika mji huo mdogo kunahitajika watu waadilifu katika ukusanyaji wa mapato ili kusaidia kutekeleza shughuli za maendeleo ya wananchi.

Aliwaagiza watendaji hao kuhakikisha shule za msingi na sekondari kwenye maeneo yao ikiwemo ya Shue ya Msingi ya Mikumi Mpya yenye upungufu wa madawati na vyumba vya madarasa kwa wanafunzi zinafanyiwa kazi kwa haraka ili kuondoka kadhia hizo.

Mwalimu Mkuu wa Shule Mikumi Mpya , Ibrahim Chemba , alisema kumekuwa na changamoto ya upungufu wa madawati na vyumba vya madarasa na kusababisha kupungua kwa ufanisi wa ufundishaji kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi kukaa chini na kubanana wakati wa kujifunza.

Chanzo: habarileo.co.tz