Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC aunda tume kifo cha mfanyabiashara

Kifo Kifo Mauiaji.png RC aunda tume kifo cha mfanyabiashara

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI mkoani Kigoma imeunda kamati kuchunguza kifo cha utata cha Mfanyabiashara wa Katoro Wilaya ya Geita, Enos Elias ambaye ni mwenyeji wa Kijiji cha Ilabiro, Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.

Kaimu Mkuu wa mkoa Kigoma, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ametoa taarifa ya kuundwa kwa kamati hiyo ya watu sita Novemba 15 mwaka huu na kuitaka kuanza kazi mara moja, huku akitoa siku saba kwa kamati hiyo kukamilisha kazi hiyo, ili taarifa hiyo iweze kufanyiwa kazi mara moja na hatua kuchukuliwa.

Marehemu Enos Elias ambaye alikamatwa na Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Kakonko Oktoba 27 mwaka huu kwa madai ya kuwa na utata wa uraia na baadaye kuhifadhiwa Kituo chaPpolisi Kakonko, ambapo baada ya hapo kumetokea utata wa mahali alipo hadi wiki moja baadaye ilipokutwa maiti yake ikiwa imezikwa kwenye pori la Kijiji cha Chilambo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live