Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC atoa wiki walioiba milioni 867/- ‘wazitapike’

7f494cba1e4856c1b94fd6bcb3312140.PNG RC atoa wiki walioiba milioni 867/- ‘wazitapike’

Thu, 24 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ameamuru watumishi walioiba zaidi ya shilingi milioni 867 wawe wamezirudisha ifi kapo Juni 30, mwaka huu.

Fedha hizo zinazodaiwa kuibwa kwenye halmashauri tano, zinakadiriwa kuweza kugharamia ujenzi wa vituo viwili vya afya. Mrindoko alitoa agizo hilo ofisini kwake wakati akiwakaribisha wakuu wa wilaya za Mlele, Mpanda na Tanganyika waliohamishiwa mkoani humo.

Alisema amefanya ziara katika halmashauri tano za mkoa huo ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Halmashauri ya Manispaa Mpanda, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Nsimbo iliyopo katika Wilaya ya Mpanda na kubaini ubadhirifu wa fedha za serikali.

Kwa mujibu wa Mrindoko, alibaini hakuna halmashauri hata moja isiyo na ubadhirifu katika mapato yanayokusanywa katika vituo vya ushuru na kuingizwa kwenye akaunti za halmashauri.

Alisema katika baadhi ya halmashauri, fedha nyingi zilitumika nje ya mifumo ya serikali au zimepotea au hazikuingizwa kwenye mfumo wa serikali.

Kaimu Katibu Tawala wa Serikali za Mitaa, Idara ya Serikali za Mitaa, Reginald Mhango, alisema baadhi ya watumishi katika Halmashauri za Mkoa wa Katavi, walipokea fedha kutoka kwenye vituo vya kukusanya ushuru kwa njia ya mfumo wa mapato, lakini hawakuziingiza kwenye mfumo wa ukusanyaji mapato wa serikali za mitaa (LGRCIS).

Mhango alisema Halmashauri ya Mlele imepokea na haijaingiza Sh milioni 457, Halmashauri ya Mpimbwe ilipokea na haijaingiza Sh milioni 52, Halmashauri ya Manispaa Mpanda Sh milioni 138, Halmashauri ya Nsimbo Sh milioni 71 na Halmashauri ya Tanganyika zaidi ya Sh milioni 149.

Mrindoko aliagiza fedha hizo zitafutwe kokote zilipo na ziingizwe kwenye akaunti za serikali ili ziweze kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz