Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC atoa ratiba ya kusajili simu kushirikisha NIDA na TCRA mkoa Arusha

90874 Pic+nida RC atoa ratiba ya kusajili simu kushirikisha NIDA na TCRA mkoa Arusha

Sun, 5 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ametangaza mkakati wa kuhakikisha wakazi wote wenye simu za mkononi Mkoani Arusha, Tanzania, wanasajili laini zao kwa alama za vidole kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida).

Gambo amesema hayo leo Jumapili Januari 5, 2020 alipozungumza jijini Arusha.

Akifafanua, Mkuu huyo wa mkoa amesema kazi ya usajili  kwa Jiji la Arusha  itafanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Januari 6 na 7, 2020 wa kuhusisha kampuni za simu, Nida na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Amesema Wilaya ya Longido, kazi hiyo itafanyika Mji wa Namanga Januari 8, Halmashauri ya Arusha litafanyika eneo la Ngaramtoni Januari 9, 2020.

Gambo amesema kwa upande wa Wilaya ya Monduli, kazi hiyo itafanyika Januari 10 katika mji wa Mtowambu, Halmashauri Meru  Januari 11 soko la Tengeru na Karatu watafanya Januari 12 kwenye Viwanja vya Mazingira Bora.

Wilayani Ngorongoro itafanyika kwa siku mbili Januari 13 Ofisi za Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro  na Januari 14 eneo la Wasso tarafa ya Loliondo.

Chanzo: mwananchi.co.tz