Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigella amezitaka halmashauri zilizopokea fedha za kusaidia jamii (CSR)kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM), kukamilisha miradi hiyo kufikia mwaka 2024.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini makubaliano ya kusaidia jamii katika halmashauri tano za mkoa huo na mgodi wa GGM, Shigella ameagiza kukamilika kwa miradi yote ndani ya kipindi hicho kwa kuzingatia ubora na thamani ya fedha.
Shigella amesema, miradi mingi ya CSR haikukamilika kwa wakati ama kutokamilika kabisa kutokana na usimamizi mbovu wa miradi hiyo kwenye halmashari hizo.
Ameongeza kuwa fedha zinazotolewa ni nyingi na zinapaswa kusimamiwa kwa ukaribu, ili ziweze kutoa matunda yanayotarajiwa kwa jamii ambayo inalengwa na msaada huo.
Kwa mwaka 2021/2022 na 2022/2023, GGM imetoa shilingi Bilioni 19 kwa ajili ya kusaidia miradi ya kijamii katika halmashauri tano za mkoa wa Geita.