Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC atoa angalizo watoto kuaga mwili Kirumba

3 8 1024x517 RC atoa angalizo watoto kuaga mwili Kirumba

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mongella alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na kamati ya maandalizi ya shughuli, kwa lengo la kuepusha vifo na madhara yanayoweza kutokea kutokana na msongamano unaoweza kusababishwa na watu wengi wenye shauku ya kuuaga mwili.

"Idara zote za ulinzi na usalama zimejipanga kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarika, na nitoe ombi kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanabaki nyumbani wakitazama kwenye runinga, kwa kuwa matangazo yanarushwa kwenye channel zote za ndani,” alisema.

Alisema Rais Magufuli ni kipenzi cha watu wa Mwanza na Kanda ya Ziwa, hivyo wanategemea  idadi ya watu kuwa kubwa, na kwamba idara zote zinajipanga pamoja na wanaohusika na sekta ya afya. Pia alisema Chama cha Msalaba Mwekundu na skauti wahakikishe wanakuja watu wazima ili waweze kusaidia pale tatizo linapotokea.

"Mageti ya kuingilia uwanjani yatafunguliwa kuanzia saa 10 alfajiri na mwili utapokelewa uwanja wa ndege saa 1:00 asubuhi ukitokea Zanzibar na utapelekwa uwanjani hapo moja kwa moja kisha sala, dua na maombezi yatafanyika,” alisema Mongella na kuendelea:

“Baadaye viongozi mbalimbali wa kitaifa na mkoa watatoa heshima zao za mwisho kisha mwili kuruhusiwa kupitishwa kwenye barabara mbalimbali za Jiji la Mwanza.”

Kwa mujibu wa Mongella, barabara ambazo mwili utapitishwa ni Makongoro, Pasiansi, Msumbiji, Mwontensori, Loreto, Buzuruga, Mabatini, Mjinj Kati, CCCM Mkoa, Igogo, Nyegezi, Mkolani, Buhongwa, Usagara, Kigongo kisha utavuka maji kwenda Sengerema.

Chanzo: ippmedia.com