Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC atangaza vita na wapigaji fedha za miradi

Mongela Mongela RC atangaza vita na wapigaji fedha za miradi

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

: Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,John Mongella amekemea tabia ya wahandisi kuletewa fedha za miradi kutoka serikalini na badala yake fedha hizo kuisha bila miradi kumalizika kisha kupanga kuongeza fedha nyingine kutoka mapato ya ndani. - Mongella amesema hayo wilayani Longido baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya kata Mundarara na kupewa tarifa ya fedha zilizotolewa na serikali kiasi cha Sh,milioni 470 kuwa hazikukamilisha mradi huo na kupanga kuongeza fedha kutoka mapato ya ndani. - Mbali na kuuagiza uongozi wa Wilaya ya Longido kukamilisha ujenzi wa mradi huo katika maeneo yaliyosalia ifikapo Desemba 15, ametaka mradi huo kuzingatia vigezo vya ubora vilivyoainishwa na serikali na kuwasisitiza kuhakikisha fedha zilizotolewa na serikali zinakamilisha mradi huo bila kuongeza fedha kutoka mapato ya ndani. - "Hii tabia ya kumaliza fedha za miradi halafu mnadai mtaongeza nyingine katika mapato ya ndani acheni na kwanini Wilaya hii mnakuwa na miradi viporo au hammalizi miradi kwa wakati, jitahimini na mjipange katika usimamizi wa majukumu yenu, sitaki miradi viporo"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live