Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC atangaza vita na waokota taka, wachimba dawa

Kuchimbadawa Stopppp RC atangaza vita na waokota makopo, wachimba dawa

Thu, 30 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (RC), Juma Homera ameagiza kuanza msako na kukamatwa watu wakiwamo wanafunzi wa shule za msingi wanaojihusisha na uokotaji wa mabaki ya vyakula na taka hatarishi katika maeneo ya kutupa taka maarufu maguba katika Jiji hilo.

Homera ametoa agizo hilo leo Alhamisi June 30,222 kwenye kikao cha wadau wa ukusanyaji, uhifadhi, usafirishaji na urejeshaji wa taka hatarishi kilichoandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa.

Amesema kuwa kumeibuka kundi la watu wanaoamka alfajiri na jioni kuzunguka kwenye maguba kuokota mabaki ya vyakula na taka hatarishi hali ambayo inahatarisha usalama wa afya zao.

''Nemc tungeni sheria ndogo za kuwabana watu hao na pia shirikianeni na Jeshi la Polisi mnapowabaini wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya dola kwani ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira na pia wana hatarisha usalama wao''amesema.

Homera amesema tabia hiyo ipo mpaka kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi ambapo wanakimbia masomo na kujihusisha na uokotaji wa taka hatarishi hivyo amesema hawezi kuvumilia katika hilo na kuagiza wakamatwe.

Katika hatua nyingine ameagiza vyombo vya dola kushirikiana na Nemc kuanza kufuatilia mabasi ya masafa marefu ambayo yamekuwa na tabia ya kusimama njiani na abiria kuchimba dawa porini.

''Kuna baadhi ya kampuni za mabasi wanaendekeza tabia ya kushusha abiria njiani na kuchimba dawa sasa hilo shirikianeni, kamateni wapitozwe faini ''ameagiza

Kwa upande wake Meneja wa Nemc Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Groly Kombe amesema Nemc wataendelea kusimamia kanuni na sheria zilizowekwa katika kutunza mazingira.

Mkazi wa Mbeya, John Haule ameunga mkono agizo la Mkuu wa Mkoa la kukamtwa wanafunzi wanaoacha masomo na kuokota mabaki ya vyakula na taka hatarishi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live