Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC ataka tathmini kukabili mimba za utotoni

2f00261e75b6a86214b4d01028106273 RC ataka tathmini kukabili mimba za utotoni

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amewaagiza wakuu wa wilaya mkoani humo kusimamia tathimini ya utekelezaji wa mkakati wa miaka mitano (2020 -2025) ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni ifi kapo Januari 2021.

Ameagiza tathmini ifanyike Januari mwakani katika ngazi ya wilaya na Februari katika ngazi ya mkoa kubaini mafanikio na changamoto yaliyobainika katika kipindi cha mwaka mmoja tangu mkakati huo ulipozinduliwa Februari 18 mwaka huu.

Alitoa maagizo hayo jana alipozindua mradi wa kuzuia ndoa na mimba za utotoni mkoani Rukwa wenye kauli mbiu ‘Tushirikiane kwa pamoja kuzuia mimba na ndoa za utotoni’ unaotekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika yasiyo ya kiserikali.

Aliagiza pia wakuu hao wa wilaya kuhakikisha shule za msingi zinajengwa katika kila kijiji na shule za sekondari katika kila kata pamoja na wazazi kuchangia chakula shuleni na ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule za sekondari “Wanafunzi kushinda na njaa, shuleni kutembea mwendo mrefu kunasababisha utoro sugu na mimba za mapema ... Mkoa wetu una vijiji 339 huku vijiji 59 havina shule za msingi lazima zijengwe kabla ya mwisho wa mwaka kesho,” alisema.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Programu wa Shirika la Plan International Tanzania, Laurent Wambura alisema ndoto za mtoto wa Tanzania zimeendelea kuathirika kutokana na kukosa nafasi ya kuendelea na masomo kwa kupewa ujauzito katika umri mdogo.

“Mradi huu umelenga kuwafikia watoto 32,167 kati yao wasichana ni 23,356 huku wavulana wakiwa 9,811 na wazazi 21,881 wanaoishi katika vijiji 116 na kata 36 katika halmashauri za wilaya za Nkasi, Kalambo na Sumbawanga,” alibainisha.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda aliliomba shirika hilo lione uwezekano wa kuziingiza katika mradi huo kata za Nkinga na Kipili kutokana na kiwango kikubwa cha mimba za utot

Chanzo: habarileo.co.tz