Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC ataka miradi ikamilike kwa wakati

029e0c573dd5568ffc6345fba4608a28 RC ataka miradi ikamilike kwa wakati

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge ametembelea miradi ya ujenzi ya barabara na madaraja na kutaka miradi hiyo isicheleweshwe kwa kisingizo cha mvua zinazoendelea kunyesha.

Miradi aliyotembelea na gharama zake kwenye mabano ni Ulongoloni A (Sh bilioni 4.3), Ulongoloni B (Sh bilioni 17), ujenzi wa barabara ya Makongo kwenda Goba kilomita 4.2(Sh bilioni 8.2) pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara ya Goba kwenda Wazo kupitia Kisauke ya kilomita 6 inayogharimu Sh bilioni 6.7.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo, alisema wapo ambao wamekuwa wakiendelea vizuri kutokana na kufanya kazi kwa mujibu wa makubaliano kwa muda husika, lakini pia wapo ambao wamekuwa wakisuasua.

“Nawaagiza wakandarasi wote wafanya kazi usiku na mchana, kuhakikisha kwamba miradi hiyo inaisha mapema. Kwao wanaona inaenda haraka, lakini kwa wananchi wanaona wanachelewa kupata huduma,”alisema.

Aidha amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Dar es Salaam(Dawasa) kuondoa miundombinu yao haraka ili kupisha ujenzi wa miradi hiyo kwa sababu tayari wameshalipwa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz