Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC ataka hamasa watoto kupewa vyeti vya kuzaliwa

473dc1d107b7232e6796be9110c93496.jpeg RC ataka hamasa watoto kupewa vyeti vya kuzaliwa

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa mkoa wa Tanga Martin Shigela amewataka wakuu wa wilaya zote za mkoa hapa kuhakikisha wanasimamia kwa ukaribu na kuhamasisha wananchi kusajili watoto wao chini ya umri wa miaka mitano ili waweze kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati kikao cha tathimini ya mpango kutoa vyeti bure vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano kwa Mkoa wa Tanga alisema kuwa licha ya kuendesha kazi hiyo lakini kasi ya uandikisha imeanza kupungua.

Alisema kuwa licha ya watoto kuzaliwa katika hospitali lakini mitaani kuna idadi kibwa ya watoto wasio na vyeti hivyo ipo haja

ya kuendelea kuhamasisha zoezi hilo ili liweze kuleta mafanikio mazuri tofauti na hapo awali.

“Tusipokuwa makini tutajikita tunarudi chini katika shughuli hiyo kwani nataka tuongeze juhudi ili ifikapo mwishoni mwa mwaka huu tuweze kusajili watoto kwa asilimia 100,” alisema Shigela.

Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu wa Wakala wa Usajili , Ufilisi na Udhamini RITA Emmy Hudson

alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kazi hiyo imeweza kuleta mafanikio makubwa kutoka asilimia nne ya watoto wenye vyeti vya kuzaliwa hadi kifikia asilimia 81.

Alisema kuwa kupitia mpango huo jumla ya watoto laki 291 walisajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa bure mwaka 2020 hata hivyo alisema mwaka huu kasi imepungua kwani katika kipindi cha miezi mitatu

wameweza kusajili asilimia mbili tuu.

“Katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu tumeweza kusajili watoto 1, 403 sawa na asilimia mbili wakati lengo ilikuwa ni kusajili zaidi ya asilimia 22, hivyo ipo haja ya kuhakikisha tunaongeza kasi ya uhamasishaji kwa jamii kuona umuhimu wa watoto wao kuwa na vyeti vya kuzaliwa,” alisema Hudson.

Chanzo: www.habarileo.co.tz