Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC asita kutekeleza agizo la naibu waziri

59070 PIC+RC

Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Mkuu wa mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema agizo la kuwakamata wakandarasi wanaojenga mradi wa maji wa Nyamtukuza wilayani Nyang’hwale atalifanyia kazi baada ya kushauriana na watendaji na wanasheria wa mkoa.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana kuhusu utekelezaji wa agizo hilo lililotolewa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso kwa uongozi wa mkoa huo kuwakamata wakurugenzi wa kampuni ya PET Co-operation Ltd na Famoyo Ltd za jijini Dar es Salaam inayotekeleza mradi huo, Gabriel alisema suala hilo linahitaji mashauriano kwanza.

“Nilikuwa safarini. Ndio nimerudi ofisini na kukuta agizo la naibu waziri. Sijalitekeleza kwa sababu nahitaji kushauriana kwanza na wasaidizi wangu wakiwamo wanasheria ili kuepuka kufanya makosa kutokana na mradi husika ulikuwa chini ya wizara,” alisema.

Gabriel alisema mradi huo ulioanza mwaka 2014 unaojengwa kwa gharama ya Sh15 bilioni uko chini ya wizara ya maji na umwagiliaji hivyo ili waweze kutekeleza agizo la naibu waziri, wanapaswa kwanza kupitia mkataba wake ili kuona masharti na taratibu zilizokiukwa.

“Lazima tuchukue tahadhari kuepuka kujiingiza kwenye mtego na makosa ya kisheria,” alisema.

Akiwa wilayani Nyang’hwale Mei 18 mwaka huu, Aweso aliagiza makandarasi hao kukamatwa na kuswekwa mahabusu kwa tuhuma za kuchelewesha mradi huo huku wananchi wakiendelea kupata shida ya maji.

Pia Soma

Alisema licha ya Serikali kutoa zaidi ya Sh400 milioni tangu mwaka 2014 ikiwa ni fedha za kianzio lakini hakuna kilichofanyika hadi sasa.

“Tangu wakati huo maji hayajatoka hata kwenye kijiji kimoja kati ya vijiji tisa vinavyotakiwa kunufaika na mradi huu, kama kuna mtu anawalinda sasa inatosha, kama mlikula fedha za umma mtazitapika,” alisema Aweso.

Mbunge wa Nyang’hwale, Hussein Kasu alisema wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo la maji licha ya Serikali kulipa mamilioni ya fedha kwa makandarasi.

Chanzo: mwananchi.co.tz