Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC asimamisha watumishi 8 mpaka wa Horohoro (+video)

Video Archive
Thu, 26 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella, amewasimamisha kazi maofisa 8 wa taasisi tatu tofauti, ikiwemo TRA, TBS na idara ya mifugo katika kituo cha forodha kilichopo mpaka wa Horohoro kwa madai ya kujihusisha na rushwa pamoja na kuisababishia serikali hasara.

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella, amewasimamisha kazi maofisa 8 wa taasisi tatu tofauti, ikiwemo TRA, TBS na idara ya mifugo katika kituo cha forodha kilichopo mpaka wa Horohoro kwa madai ya kujihusisha na rushwa pamoja na kuisababishia serikali hasara. Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara waliyoyatoa kwa RC Shigella, kuwa vitendo vya rushwa vimekithiri katika ofisi za watumishi wa serikali katika boda hiyo, na ndipo alipoamua kuunda kamati maalumu ya uchunguzi iliyoanza kazi yake Novemba 18 kwajili ya kuchunguza mwenendo wa watumishi hao.“Hapa wamegeuza kuwa ni shamba la bibi, hawa wanaenda kwenye taratibu za kiuchunguzi na vyombo vya dola viwachukue wakaanze kutoa maelezo kwanini wasipelekwe mahakamani, na hapa waletwe watumishi wengine tunataka kituo cha Horohoro kiwe cha mfano kwa kuhudumia wateja” RC Shigella

Chanzo: millardayo.com