Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC aonya watumishi kuwavuruga madiwani

3cffb57bfb305bad10f9e5babdec9f1a RC aonya watumishi kuwavuruga madiwani

Thu, 17 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WATUMISHI wa halmashauri ya wilaya ya Hanang,mkoani Manyara wametakiwa kuacha tabia ya kuwavuruga madiwani kwa kutoa ushauri usio faa huku wakitoa huduma kwa upendeleo kulingana na diwani anayeelewana nae.

Aliyasema hayo Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti katika kikao cha kuwaapisha madiwani na kuchagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa halmashauri.

Mkirikiti alisema mtumishi yeyote atakayebainika kuwa na tabia za kuwavuruga madiwani kwa namna yoyote ile watahakikisha wanamshughulikia ili kukomesha tabia hiyo kwani vitendo hivyo ni ukwamishaji wa shughuli za maendeleo.

"Hawa watu ni watu wenye busara sana,tumehangaika nao sana toka kipindi cha kampeni mnajua, ziko tabia za watumishi baadhi yenu kuwavuruga madiwani mnajua,nawaomba watumishi wa hapa isitokee hiyo tabia".

Mkirikiti alimpongeza diwani wa kata ya Basutu, Rose Kamili kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye alishinda kwa kura 43 kati ya kura 45 zilizopigwa ambapo wilaya ya hanang inaundwa na kata 45.

Katika nafasi zote mbili za kugombea uenyekiti na makamu mwenyekiti hapakuwa na wagombea kutoka vyama vingine vya upinzani hivyo kila jina lilipigiwa kura ambapo kura zote zilikuwa zinafanana hali inayopelekea Rose Kamili kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo na Willium Manase ambaye aligombea umakamu mwenyekiti kuwa makamu Mwenyekiti kwa muda wa mwaka mmoja.

Halmashauri hiyo inayoundwa na kata 45 imefanikiwa kusimamisha madiwani wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) 43 huku kata mbili za Balagdalalu na Dumbeta zikichukuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Akizungumza baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti, Rose Kamili ambaye alikuwa Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa muda wa miaka 10 na baadaye kuamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) alisema kuwa atahakikisha anatoa ushirikiano kwa madiwani wote bila kujali nani amempigia kura.

Aidha alisema atahakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo na kusimamia fedha zinazoletwa kutoka serikali kuu pamoja na kusimamia upatikanaji wa mapato ya ndani ya halmashauri hiyo; hivyo akawataka kila diwani katika kata yake kuhakikisha anasimamia mapato hayo.

Chanzo: habarileo.co.tz